Mamia ya watu wamejitokeza nchini
Tanzania kumuaga marehemu Captain John Komba, mbunge na msanii maarufu
wa uhamasishaji aliyefariki siku ya Jumamosi.
Captain Komba
atakumbukwa kwa uhodari wake katika kuimba nyimbo za kuhamasisha
wananchi katika mambo mbalimbali hasa ya kisiasa kwa niaba ya chama
chake cha CCM.Mpaka anafariki alikuwa mbunge wa jimbo la Mbinga
Magharibi. Kando na siasa, Komba alishiriki katika uhamasishaji wa
jamii mfano wimbo wa ‘Mgeni’ uliokuwa ukitoa elimu juu ya ugonjwa wa
UKIMWI.
Kundi la mziki tanchy linaloudwa nao Chibwa na Tanah wameachia video ya wimbo wao ujulikanao kwa jina la "Mabawa" , Video imeongozwa nae marijani pata kuitazama hapa........
Mkali wa miondoko ya hip hop fid q ameachia rasim video ya nyimbo yake ambayo iliombwa na mashabiki wake kabla hajaachia nyimbo nyingine kutoka kwake. Fid Q ameonesha mfano mzuri kwa kuwasikiliza mashabiki wa mziki wake nini wanakihitaji kwa muda sahihi. Maneno hayo ameyazungumza Fid Q mwenyewe katika kipindi cha XXL cha clouds Fm, Video imeongozwa nae Nisha director anaye kuja kwa kasi kwenye tasinia ya mziki nchini....
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid
Benz' baada ya kulipa faini, Awali msanii huyo alipewa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini kufuatia kukamatwa akiwa na
madawa ya kulevya. Chid
Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo
misokoto ya bangi. Mwanamuziki
huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo
akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la
muziki.
Daada ya kimya cha mda mrefu hatimae Dulayo msanii wa mziki wa miondoko ya bongo freva ameachia wimbo wake mpya aliomshlikisha prof J. wimbo inakwanga kwa jina Mokomoko