Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Thursday, 26 June 2014

Gavana wa Lamu Kenya amekamatwa kwa mahojiano na maafisa wa polisi

Gavana wa Lamu Kenya amekamatwa

Maafisa wa polisi wakifanya doria
Polisi nchini kenya wamemtia mbaroni gavana wa jimbo la Lamu lililokumbwa na mapigano hivi majuzi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 65.
Polisi walimshika Issa Timamy,kufuatia tuhuma za kuhusika na mashambulizi yaliyotokea Mpeketoni mapema mwezi huu.


Timamy anatarajiwa kufikishwa mahakamani mjini Mombasa alhamisi.
Punde baada ya tukio hilo rais Uhuru Kenyatta alikatalia mbali madai kuwa ilikuwa shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na kundi la waislamu la Al shabab.

Haya ndio baadhi ya mabaki ya magari yalio kuwapo eneo la tukio
Rais Kenyatta alisema kuwa hilo lilikuwa shambulizi lenye misingi ya kikabila na kisiasa.
Kundi la wapiganaji kutoka Somalia Al shabab lilidai kutekeleza shambulizi hilo.
Bwana Timamy ni Gavana wa pekee kutoka chama cha UDF .

Sehemu halisi tukio lilipo tokea
Rais Kenyatta alipinga kuhusika kwa Al shabab kwani wengi waliouawa walikuwa wa jamii ya wakikuyu jamii anayotoka rais Kenyatta .
Aidha wavamizi waliwalenga wanaume ambao hawakuwa waislamu na kuwataka kukariri shahada ama aya za Quran,wale walioshindwa walikuawa .
Siku ya jumatano maafisa wa utawala katika jimbo hilo la Lamu walidai kuwa wamewakamata watu 13 waliokuwa wakipanga njama ya kufanya uvamizi zaidi.