Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Monday, 21 July 2014

HATIMAYE MSHAMBULIAJI WA YANGA JAJA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI.......


Jaja akipokea nakala ya mkataba wake kutoka kwa Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu
leo maraa baada ya kusaini kuitumikia kwa miaka miwili
Hatimaye mshamabuliaji Geilson Santos Santana "Jaja"  raia wa Brazil leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2014-2016) kuitumikia timu ya Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

Katibu mkuu wa Young Africans  Bw Beno Njovu amesema usajli wa Jaja unakua ni wa pili msimu huu kwa wachezaji wa kimataifa baada ya awali kumsajili kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia ni raia wa Brazil.
"Kazi yetu uongozi ni kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi, walitoa mapendekezo ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi" alisema Beno.

Jaja ambaye alizaliwa tarehe 21 Septemba 1985 na kukulia katika mji wa Aracaju nchini Brazili mpaka anasajiliwa na timu ya Young Africans alikuwa akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo mwenye mwili uliojaa vizuri tayari alishaanza mazoezi tangu katikati ya wiki iliyopita chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo na msaidizi wake Leonado Neiva ambao wanaendelea kukinoa kikosi cha Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali.