Liverpool imekubali kumuuza mshambulizi wake Luis Suarez kwa Barcelona kwa kima cha pauni milioni 75.

.
Suarez anasema kuwa yeye pamoja na familia yake, daima watakuwa mashabiki wa Liverpool.Suarez alikuwa mfungaji mabao mengi zaidi katika msimu uliopita na mshindi wa tuzo la mchezaji bora . Alitia saini mkataba na Liverpool alipotoka Ajax mwaka 2011 kwa pauni 22.7.