Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo (Jumatano) asubuhi.
Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Edward Lowassa ametembelea shule hiyo na kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.
Gharama za kuwasafirisha wanafunzi hao ni shilingi laki Saba. Aidha Mh Lowassa amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
Kikosi Cha zimamoto kikijaribu kupambana na moto ulioteketeza mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo Monduli mjini yaliyoteketezwa kwa moto.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa afisa elimu wa Monduli mwalimu Shaaban Mgunya wakati alipotembelea mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli yaliyoteketea kwa moto.