Moto ambao Madhara yake yanayonekana kwa sasa ni pamoja na kuteketeza nyumba ya vyumba 12 pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani ya vyumba,pamoja na vyumba 4 vya biashara vilivyopo nje ya barabara.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondon kamishna msaidizi wa polisi Camellius Wambura amethibitisha kutokea kwa moto huo na kusema Moto huo umetokea leo majira ya saa 5 na nusu mtaa wa Malanga eneo la Mwanayamala.
Nyumba iliyotoketea kwa moto imetajwa mmiliki wake kuwa ni mzee abdalah, ambaye alikuwa akimiliki nyumba mbili zilizopakana katika eneo hilo zote zikiwa zina vyumba 12,chanzo cha moto huo kinasemekana ni hitilafu ya umeme.
Wananchi wa eneo hilo wamelalamikia hali ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kuchelewa kufika eneo la tukio.
Baadhi ya picha katika tukio hilo
source:millardayo.com