Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli,
24, amekamilisha uhamisho wake kutoka AC Milan kwenda Liverpool kwa
pauni milioni 16. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City, amekubali
mkataba wa muda mrefu, ingawa hatoweza kucheza dhidi ya timu yake ya
zamani Jumatatu usiku. Balotelli aliondoka City miezi 17 iliyopita baada
ya kupachika mabao 30 katika misimu mitatu.
"Uhamisho huu unawakilisha misingi ya klabu na nadhani tumefanya biashara nzuri tu hapa," amesema bosi wa Liverpool, Brendan Rodgers. Balotelli, ambaye atavaa jezi namba 45, amesema alifanya makosa kuondoka England mwaka jana. "Nimefurahi kurejea tena, kwa sababu nilifanya makosa kuondoka England," amesema na kuongeza "Nilitaka kwenda Italy, lakini nikagundua ni makosa."