Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid
Benz' baada ya kulipa faini, Awali msanii huyo alipewa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini kufuatia kukamatwa akiwa na
madawa ya kulevya.
Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo misokoto ya bangi.
Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.