Mfungo huo ambao ni wa siku 30 ilianza Jumapili na kocha Halilhodzic, mwenye umri wa miaka 61, alikataa kujibu swali ikiwa wachezaji wake watafunga Ramadhan au la wakati wakicheza.
"hili ni swala la kibinafasi na unaponiuliza swali hilo basi unaonekana kukosa nidhamu na heshima, '' alijibu kocha huyo raia wa Bosnia.
Mfungo wa Ramadhan ni sharti kwa kila muisilamu na ni moja ya nguzo za imani yua dini ya kiisilamu, ingawa wagonjwa na wazee wanaruhusiwa kutofunga.
Watu ambao wanasafiri au kuenda vitani pia wanaruhusiwa kujiepusha na kufunga na hii ni moja ya sababu ambazo wanamichezo hukosa kufunga hadi wanapokamilisha shughuli zao.
Bila shaka ni swali ambalo lilimuudhi kocha Halilhodzic. ''Nimesoma katika baadhi ya magazeti nchini Algeria yakinikosoa na kunichafulia jina.Wanajaribu kuzua chuki kwa familia yangu , kwangu mimi na hili linanichukiza sana, '' alisema kocha huyo kwa hasira.
Bila shaka ni swali ambalo lilimuudhi kocha Halilhodzic. ''Nimesoma katika baadhi ya magazeti nchini Algeria yakinikosoa na kunichafulia jina.Wanajaribu kuzua chuki kwa familia yangu , kwangu mimi na hili linanichukiza sana, '' alisema kocha huyo kwa hasira.
"sio mara ya kwanza kwangu kuwa na wachezaji waisilamu katika timu ya mpira. Mimi mwenyewe ni Muisilamu na mimi huwaacha kuwa huru wachezaji kuamua wanachotaka. Hili ni swala la kibinafsi. ''
"kwa wale wanaoendelea kukosoa timu hii na wachezaji nadhani ni jambo la aibu sana. Lakini nitaendelea kuwa na wachezaji hawa, na ni jambo la kusikitisha kuwa mnaendelea kukosoa timu yangu kila wakati. ''
Kinara wa timu hiyo, Madjid Bougherra, ameeleza kuwa atafunga ingawa mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil na mchezaji wa Ufaransa Bacary Sagna ambao ni waisilamu wamesema hawatafunga
SOURCE BY BBCSWAHILI
SOURCE BY BBCSWAHILI