EVANS Aveva amechaguliwa kwa kishindo kuiongoza Simba katika uchaguzi mkuu uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, huku mashabiki na wanachama wa Msimbazi wakiimba kwa furaha kwamba wamempata rais kiboko ya Yanga na kocha wao mpya, Marcio Maximo ‘The Chosen One’.
Aveva katika kampeni zake aliweka bayana na hata jana alisisitiza kwamba wanachama wamkabidhi uongozi aimalize Yanga.
Matokeo ya awali kwa mujibu wa watu waliokuwa chumba cha kuhesabia kura Aveva amepata 1452 huku mpinzani wake Andrew Tupa akipata kura 386 na kura sita zikiwa zimeharibika.
Kwa Makamu wa Rais, hadi tunakwenda mitamboni Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alikuwa amewashinda Swedy Mkwabi, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Bundala Kabulwa. Kura za wajumbe zilikuwa zinaendelea kuhesabiwa.
Kwa wajumbe hadi tunakwenda mitamboni washindi walikuwa ni Said Tully, Idd Kajuna, Jasmin Sudi na Collins Frisch.
Wambura azuiwa
Wambura alienguliwa na Kamati ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake, Damas Ndumbaro baada ya kufanya kampeni kabla ya wakati.
Awali kamati hiyo pia ilimwengua kwa madai kuwa hakuwa mwanachama halali wa Simba, baada ya kusimamishwa uanachama mwaka 2010 alipopeleka masuala ya soka mahakamani, kabla ya Kamati ya Rufaa ya TFF kumrejesha tena.
Katika Uchaguzi Mkuu wa Simba mwaka 2010, Wambura alienguliwa kugombea nafasi ya mwenyekiti baada ya kufungua kesi katika mahakama ya Kisutu kuushtaki utawala wa aliyekuwa Mwenyekiti Hassan Dalali jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya TFF, Caf na Fifa. Katiba hizo zinakataza kupeleka mashauri ya soka mahakamani.
Katika uchaguzi huo wa jana Wambura alifika katika ukumbi huo kwa lengo la kutimiza haki yake ya msingi ya kuchagua viongozi wapya wa klabu hiyo lakini Kamati hiyo ya Uchaguzi ilimwekea ukuta na kuishia kuchungulia wanachama wengine wa klabu hiyo waliokuwa ndani ya bwalo hilo.
Akizungumza mara baada ya kukutana na kisiki hicho, Wambura alisema, “TFF walisha
SOURCE MWANASPORT
SOURCE MWANASPORT