Marufuku ya utafunaji wa miraa
nchni Uingereza inaanza kutekelezwa leo, nchini Uingereza. Mmea huo
hutafunwa na watu wengi wenye asili ya kisomali , Yemen na Ethiopia,
Serikali ya Uingereza inasema kuwa kuharamishwa
kwa Miraa nchini Uingereza inaambatana na hatua zilizochukuliwa na
mataifa mengine ya Ulaya pamoja na Marekani ambako Miraa ni haramu.
Watumiaji wa mmea huo wanasisitiza
kuwa sio hatari kuutumia na kwamba kuupiga marufuku ni ubaguzi dhidi ya
jamii ambazo ni za wachache.
Mmoja wa watu ambao wamekuwa wakiutumia mmea
huo, Aden Haj anasema alitelekezwa na familia yake ambayo haingeweza
kustahamili utumiaji wake wa Miraa na anawataka watu kufahamu athari za
kutumia Miraa.
Nchini Kenya ambako mmea huo unakuzwa, maelfu ya
wakulima katika eneo la Meru sasa wanakabiliwa na tishio la kupoteza
mamilioni ya pesa baada ya marufuku ya kusafirisha miraa nchini
Uingereza kuanza kutekelezwa.
Hatua hiyo inajiri baada ya Uingereza
kuharamisha utafunaji wa miraa nchini humo baada ya mmea huo
kuorodheshwa miongoni mwa madawa ya kulevya.
Uingereza ni mojawepo wa mataifa ya bara Ulaya
yaliyokuwa yakitoa soko kubwa zaidi kwa zao la miraa kutoka Kenya
kutokana na idadi kubwa ya watu wa jamii ya wasomali wanaoishi nchini
humo.