Shirika la kupambana na madawa ya kulevya nchini Kenya, NACADA, limeharamisha ladha kumi na tisa za Shisha.
Kwa mujibu wa afisaa mkuu mtendaji wa shirika
hilo Fazul Mohammed, shirika hilo kwa ushirikiano na wanasayansi wa
serikali waligundua kuwa ladha hizo wakati mwingi zinakuwa
zimechanganywa na madawa ya kulevya kama vile Cocaine na Heroine.Baadhi ya ladha hizo pia ziligunduliwa kuwa na Bhangi.
Ladha hizo ambazo zinapaswa kuondoshwa sokoni mara moja ni pamoja na Al Fakher yenye ladha ya strawberry , Al Fakher yenye ladha ya chungwa , Al Fakher yenye ladha ya tufaha, Al Fakher vanilla , Al Fakher Mapera, Al Fakher appeals, Al Fakhar chungwa ikiwa na ladha ya mint na nyinginezo.
Kwa mujibu wa Bwana Fazul , kwa wale watakoapatikana wakitumia Shisha lenye ladha hizo ambazo zimepigwa marufuku, watashitakiwa.
Mwenyekiti wa tume ya shirika hilo, John Mututho, amenukuliwa akisema watakaopatikana wakiuza au kutumia bidhaa hizo, watafikishwa mahakamani.