Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Thursday, 26 June 2014

Majambazi baada ya kuuwa nayo yauwawa mkoani Geita

 Baadhi ya wanakijiji baada ya tukio
Jeshi la polisi mkoani Geita limefanikiwa kuwauwa watu wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi baada ya kupora na kufanya mauaji ya mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Gosbert Walwa katika eneo lake la biashara.


Ni majira ya saa kumi na mbili kasoro robo watu wanaosadikika kuwa ni majambazi walivamia duka la wakala wa vinywaji ambapo walipora fedha kiasi cha shilingi millioni moja na laki nane  na bastola moja  aina ya piyutro bereta yenye namba h 04788 yenye usajili wa namba 5808 iliyokuwa inamilikiwa na Ignas  Athanas na hatimaye kwenda katika vibanda vya huduma za fedha kwa njia ya simu majira ya saa kumi na mbili  na kupora fedha kiasi ambacho hakijafahamika na kufanya mauaji.
Baada ya masaa mawili kwa ushirikiano wa wananchi na jeshi la polisi, majambazi waliuwawa katika msitu wa miyenze kilomita hamsini na nane kutoka Geita mjini,mafanikio ya kuwadhibiti wahalifu hao yamewafurahisha wananchi na kuahidi kutoa ushirikiano, barabara za mji zilifurika watu mbalimbali wakishangilia vifo vya majambazi hao na kulipongeza jeshi la polisi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita  Acp Joseph Konyo amewataka wananchi kuendeleza ushirikiano uliopo kwa jeshi la polisi ambapo baadhi ya wananchi wameahidi kutoa pikipiki mpya kumi na mbili na zaidi ya shilingi millioni tatu kama sehemu ya kulipongeza jeshi hilo.