Shughuli za uokozi zikiendelea baada ya ndege ya mizigo kuanguka jijini Nairobi
Watu wanne akiwemo Rubani wa ndege moja ya mizigo, wamefari dunia baada ya ndege walimokuwemo kuanguka mapema leo asubuhi katika eneo la Utawala- Embakasi jijini Nairobi.Kwa mjibu wa shirika la msalaba mwekundu Nchini Kenya, ndege hiyo ilianguka dakika chache tu baada ya kupaa kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba SHEHENA ya Miraa ama milungi kuelekea Mogadishu Nchini Somalia.Barabara ya Estern Bypass jijini Nairobi imefungwa kwa muda huku msongamano mkubwa wa magari ukishuhudiwa.
SOURCE BY BBCSWAHILI