Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Wednesday, 2 July 2014

Riport ya daktari : Pistorius yumo katika hatari ya kjitoa uhai


Ripoti ya daktari wa magojwa ya akili iliyowasilishwa katika kesi dhidi 
ya mwariadha mashuhuri afrika ya kusini, Oscar Pistorius, inaashiria kuwa
anaugua msongo wa mawazo na yumo katika hatari ya kujitoa uhai
Ripoti hiyo iliyowasilishwa na wakili wake, inasema anamuomboleza mpenzi wake Reeva Steenkamp.Anakana kutekeleza mauaji hayo, akieleza kuwa ilikuwa bahati mbaya alipohofia kwamba aliingiliwa nyumbani mwake na mtu asiyemjua.Siku ya Jumatatu, mahakama ilielezwa kwamba Pistorius hana matatizo ya akili wakati alipompiga Bi. Steenkamp risasi .
Siku ya Jumanne, Peet van Zyl alisema Pistorius amekuwa mtu anayejulikana kimataifa katika mashindano ya olimpiki kwa walemavu ya mwaka 2012, na alitarajiwa kufanikiwa zaidi.Mwanariadha huyo aliyekatwa miguu yake miwili, alishindana katika mashindano hayo ya walemavu na ya olimpiki huko London.Van Zyl amesema huenda Pistorius angejiongezea kipato chake mara tano au sita zaidi.
Aliongeza kwamba ni mfanyabiashara na ana nafasi nyingi kutokana na kusifika kwake.Mwandishi wa BBC anasema Pistorius akiwa kizimbani Pretoria, ni hakika kwamba aliyatafakari yaliokuwa yakisemwa na Van Zyl kuhusu uwezekano wake kufanikiwa zaidi ambao kwa sasa umebadilika.Mwendesha mashtaka Gerrie Nel amesema hakujuwa kwamba Van Zyl angeitwa mahakamani kutoa ushahidi na ameomba mahakama isitishe vikao hadi Jumatano ili ajitayarishe kumhoji, ombi ambalo jaji aliliridhia.
Bwana van Zyl ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa utetezi kuwasilishwa.Mwandishi wetu anafahamu kwamba huenda upande wa mashtaka baadaye ukamuita daktari huyo, aliyemchunguza Pistorius katika mwezi uliopita, aje atoe ushahidi
Madaktari watatu wa mgonjwa ya akili waliiwasilisha ripoti moja iliyosema mwanariadha huyo yupo sawa kiakili kuendelea na kesi yake.