Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imewataka baadhi ya wanachama wake walioonesha nia ya kuomba ridhaa ya chama kugombea Urais, wazingatie katiba, kanuni na taratibu za chama hicho ili wasipoteze sifa za kugombea.
Source: Timesfm
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Katibu wa halmashauri kuu ya Taifa itikadi na uenezi ya CCM, Nape Nnauye
Katika hatua nyingine kamati kuu hiyo ya (CCM), imevipongeza vyama vya upinzani vya CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na vyama hivyo kuhusu suala la bunge la katiba.
Mazungumzo hayo yanayosimamiwa na msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi yana lengo la kuangalia kwanini baadhi ya wajumbe wa bunge maalum la katiba walisusia vikao na kutoka nje katika awamu ya kwanza ya bunge pamoja na kuangalia namna vyama hivyo vitakavyorejea katika mchakato huo kwa awamu ya pili mwezi ujao
Nape amesema ufike wakati wajumbe wa vyama hivyo waliopo katika bunge maalum la katiba watambue kuwa waamuzi wa mwisho wa mchakato huo ikiwemo idadi ya serikali ni wananchi hivyo hakukuwa na sababu ya kususia vikao vya bunge hilo.