Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Friday, 18 July 2014

Sikia hii: Baadhi ya wanakijiji wilayani makete wadai Bangi kuharalishwa

 
Watu wa Makete hutumia mbegu za Marijuana kukaangia chakula tangu zamani
Huku harakati za kutaka matumizi ya Bangi kuhalalishwa zikishika kasi katika sehemu mbali mbali duniani, Tanzania haijaachwa nyuma.
Wanakijiji katika wilaya ya Makete , mkoa wa Njombe Kusini Magharibi mwa Tanzania wanataka serikali iweke sheria ambayo itaweza kuhalalisha matumizi ya mmea huo.
Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka amesema matumizi ya Bangi katika wilaya hiyo hayajaanza leo, tangu zamani watu kitamaduni walikuwa wakitumia Mbegu za Bangi kukaanga na chakula.Wanakijiji hao zamani walikuwa wakitumia mbegu za mmea huo kukaanga na chakula lakini siku hizi wanalazimika kuzitumia kwa usiri mkubwa wakihofia kukamatwa na polisi.
Na kama mmea huo ungekuwa na athari kubwa kiafya, basi watu wengi wilayani humo wangekuwa vichaa. Miti ya mimea hiyo pia ilikuwa ikitumiwa kutengeza kamba ambazo anasema zilikuwa za nguvu sana.
Lakini kwa sababu ya sheria kali, matumizi ya Bangi au Marijuana yanafanywa kichinichini katika wilaya hiyo.

Source: BBC

Ushauri na maoni 
Askari wa jesi la polisi huteketza mashamba ya bangi nchini kote kama wakipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema . Hivyo ni budi wananchi kushirikiana na jeshi la polisi katika kutokomeza uzalishaji wa bangi ili ku nusuru kizazi cha sasa na badae hayo ni maoni yangu kama blogger.
B