Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kitengo cha habari cha Nigeria, Mike Omer, msichana huyo alikuwa kati ya wasichana watatu wanaodhaniwa kuwa members wa kundi la Boko Haram waliokamatwa usiku wa Jumanne, July 29 mwaka huu.
Ameeleza kuwa msichana huyo alikuwa na mkanda uliozungukwa na mabomu yanayotumiwa na watu wanaojitoa mhanga.
Omeri ameviambia vyombo vya habari kuwa wasichana wote watatu walijaribu kutoroka baada ya kuona polisi lakini polisi walifanikiwa kuwadhibiti.
Ametoa angalizo kwa wazazi kuwa karibu zaidi na watoto bila kujali umri i na kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu shughuli zote zinazofanywa na watoto hao.
Tukio hilo limetokea wakati ambapo bado kundi la Boko Haram linawashikilia wasichana zaidi ya 200 lililowateka April mwaka huu.