Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania
leo imepokea taarifa kutoka ubalozi wa Libya nchini ikieleza kuwa
aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya Bw. Ismail Nwairat, amefariki dunia jana
kwa kujipiga risasi.
Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya
saa saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa
Libya ambapo imeelezwa kuwa marehemu alijifungia ofisini na
kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlio wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini na kuamua kumkimkimbiza hospitali ya AMI iliyopo Oysterbay ambako alitangazwa kuwa amekwishafariki dunia, kifo ambacho kimethbitishwa pia na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu Nwairat umehamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili na kwa sasa ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wake kwenda nchini Libya kwa mazishi.