Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Monday, 21 July 2014

Sikia Ushauri kutoka kwa Mad Ice kwenda kwa wasanii hapa Bongo.........

Mad Ice awashauri wasanii kujisajiri kama kampuni ili wakopesheke, hupokea pesa kupitia copyright society ya FinlandKilio cha wasanii wa Tanzania kutokopesheka katika mabenki nchini kupitia kazi zao za muziki kilitajwa kwa uchungu na baadhi ya wasanii waliohudhuria semina iliyoongozwa na David Banner, Terrence J, Chaka Zulu na Ravi Shelton wiki iliyopita.
Mwimbaji wa muziki wa Taarabu Mzee Yusuf alitoa mfano wa ahadi zilizoshindwa kutekelezwa na benki mbalimbali nchini pale alipotaka kupewa mkopo kama bendi ya Taarabu kwa ajili ya kujiendeleza zaidi huku akitupia lawama mfumo huo.
Hata hivyo, Mad Ice aliungana na mdau mmoja wa muziki na kueleza kuwa hakuna nchi inayowakopesha wasanii fedha kama wanamuziki binafsi labda kama wataweka mali zao binafsi na kwamba njia pekee ya kupata mikopo ni kujiandikisha kama makampuni.

“Naishi Finland na system ni vilevile, mara ya kwanza ni 2004 nimeenda kuomba mkopo kwa project fulani lakini waliniambia kwamba nikienda as a company watanipa mkopo lakini wewe kama wewe msanii itakuwa vigumu. Kwa hiyo tusizilaumu hizi benki sana kwa sababu na wao ni wafanyabiashara na wanahitaji kuwa na dhamana fulani. Kwamba hii ni kampuni, inadhamana fulani, na kama wakishindwa kulipa kuna hii asset…” Amesema Mad Ice.
Alisema yeye binafsi tayari ameshajiandikisha kama kampuni na anaweza kupata mkopo.
Aliongeza kuwa wasanii wanapaswa kujiandikisha COSOTA ili mfumo utakapokaa vizuri waweze kupokea malipo ya kazi zao kutoka katika nchi mbalimbali kupitia taasisi hiyo.
“Tukienda kwenye suala la Copyright..wenzetu wakija watatuelimisha zaidi. Lakini  nimeona kwa wenzetu na mimi ni mmojawapo, kuanzia mwaka 2004 napokea pesa kila nusu ya mwaka. Napokea pesa kutoka nchi mbalimbali kupitia Copyright Society ya Finland.” Alifafanua.
Alitoa wito kwa wasanii kujiweka sawa na kuiambia COSOTA mpango wao ili mwisho wa siku mambo yaende sawa.
“Wasanii wengi hapa hawajajisajiri halafu wanalalamika..”

Source: Timesfm