Uganda itaanza utengenezaji wa magari mwaka wa 2018, imetangaza
serikali ya Uganda. Profesa Sandy Stevens, ambaye ni afisa mkuu wa mradi
unaopanga kuanzisha uundaji wa magari hayo, anasema ifikap mwaka huo
kila kitu kitakuwa tayari kuanza kazi hiyo.
Mhandisi mkuu wa mradi huo Isaac Musasizi anasema watahitaji dola za
kimarekani milioni 350, kupanga kila kitu pamoja na kujenga kiwanda cha
uundaji wa magari hayo. Anasema pia magari yakakayo kuwa yakiundwa na
nchi hiyo, ni sawa na lile lililozinduliwa na rais wa nchi hiyo Yoweri
Museveni, mwaka wa 2011.
Waziri wa biashara na viwanda nchini humo Amelia Kyambadde, anasema
kuanza kwa mradi huo wa uundaji magari ni moja wapo ya mipango ya
serikali yake, ya kuipa nchi hiyo maendeleo ya kiuchumi. Hata hivyo
serikali ya Uganda inasema itashirikiana na kampuni moja ya Kimataifa,
ili kuhakikisha magari yao yanatambulika kimataifa pindi tu yatakapoanza
kuuundwa.