WATU 42 wamejeruhiwa vibaya na 21 kati yao wakiwa na hali mbaya, baada ya gari waliliokuwa wakisafiria likitokea Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam kupata ajali katika eneo la Mchinga mkoani Lindi.
Kwa mjibu wa shuhuda habari zinasema ajali hiyo imetokea wakati dereva wa basi la SB (ambaye hajatambuliwa jina) alipotaka kupishana na lori na kusababisha ajali.
Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renatha Mzinga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema ajali hiyo ilitokea mida ya saa tano asubuhi baada ya dereva wa gari hilo ambaye ni mmoja wa majeruhi kutaka kupishana na gari jingine lilililokuwepo barabarani.
“Huyu dereva wa basi lenye namba T607 BGD alikuwa anataka kupishana na lori lililokuwepo katika barabara hiyo ambayo ni nyembamba kidogo na hivyo yeye ilimfanya apande tuta la mchanga lililokuwepo katika eneo hilo na kusababisha gari kulala upande mmoja hadi kuanguka” alisema Mzinga.
Amesema majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine.
SOURCE FIKRA PEVU