Hatua hii imeafikiwa baada ya maafisa wa serikali kuwaondoa wasimamizi wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF ofisini.
Marufuku hii inamaanisha hakuna klabu yeyoye ya soka nchini Nigeria inaweza kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa.FIFA ilikuwa imeionya Nigeria kuwa ingeichukulia hatua ifikiapo Jumanne kama Shirikisho la NFF halijarejeshewa madaraka yao lakini Serikali ikapuuza makataa hayo.Mwishoni mwa juma Serikali ya Nigeria ilikuwa imemteua afisa mshikilizi kuongoza shirikisho hilo hadi uchaguzi wa huru na wa haki utakapofanyika kulingana na taarifa ya wizara ya michezo.
FIFA katika taarifa imeonya kuwa marufuku hiyo itaondolewa tu iwapo maafisa waliochaguliwa watarejeshwa mamlakani.
Msemaji wa serikali hata hivyo alisema kuwa hatua iliyochukuliwa dhidi ya NFF ilifuata kanuni kwani hata kiongozi wa shirikisho la soka la Nigeria Aminu Maigari alikamatwa na polisi punde baada ya kurejea nyumbani kutoka Brazil.Mahakama ya Nigeria ilikuwa imeamua kuwa Maigiri hakuwa anastahili kuendelea kuiongoza NFF haswa baada ya matokeo duni huko Brazil.
Wajumbe wa NFF waliafiki kauli ya mahakama ya kumn'goa mwenyekiti huo madarakani lakini lakini kwa sasa serikali ya Nigeria inasubiri mawasiliano kutoka FIFA baada ya kutuma ithibati ya mkutano maalum uliofanyika na wajumbe wa shirikisho la soka la NFF .Mabingwa hao wa Afrika walishindwa katika mkondo wa pili wa kombe la dunia na Ufaransa .Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa timu hiyo kufuzu kwa mkondo wa pili baada ya kufuzu mwaka wa 1994 na 1998.
source by bbcswahili