Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Tuesday, 5 August 2014

Sikia hii: Wazazi wamtelekeza mtoto mgonjwa wa akili...........

 Familia moja kutoka Australia imekanusha kumtelekeza mtoto waliomlipa mama mmoja nchini Thailand kuwabebea kufuatia ripoti za daktari kuwa alikuwa na upungufu wa kiakili.
Pattharamon Chanbua, 21, aliingia mkataba wa kuwasaidia Waaustralia hao kupata mtoto baada ya mwanamke huyo kushindwa kubeba mimba mwenyewe.
Hata hivyo alipojaaliwa akazaa mapacha wazazi hao walikuja wakamchukua mmoja ambaye akili zake zilikuwa timamu na wakamuacha nyuma mtoto Gammy baada ya ripoti ya daktari kuonesha kuwa alikuwa na akili taahira.

Chanmbua anasema kuwa punde baada ya madaktari kugundua kulikuwepo na hitilafu wazazi hao wa Gammy walimshauri aavye mimba hiyo lakini akkataa kwani haiambatani na dini yake ya Kibudhaa.
Wazazi hao wa Gammy wamejitetea wakisema kuwa walimchukua mtoto mmoja baada ya madaktari kutarajia kuwa Gammy angekuwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo na maambukizi ya mapafu.
Baba ya mapacha hao wawili aliwatembelea wote wakiwa hospitalini punde baada ya kuzaliwa lakini haijulikani kwanini alimtelekeza Gammy.
Mama huyo ambaye tayari yuko na wanawe wawili sasa anasema hatamtupa Gammy bali atamlea kama mwanawe.
Matukio hayo yamepelekea watu kote nchini Australia wanakotoka wazazi wake kufoka wakiwalaumu kwa kumnyima haki zake Gammy .
Aidha wengi wanakashifu matukio hayo wakidai kuwa huo ni ukoloni mamboleo kwa watu wenye hela lakini wanamatatizo ya kuwapata watoto wao wenyewe wanasafiri kuelekea nchi za mbali na kukodisha wanawake maskini kwa niya ya kujitoa mzigo wa ukosefu wa watoto.
Mtoto aliyezaliwa na akili taahira kwa mama wa kupanga .
Lakini wakipata watoto hao wanakasoro fulani wanatoroka na kuwaachia wale wazazi maskini na mzigo wa kuwalelea watoto wao.
Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott na waziri wa maswala ya uhamiaji nchini humo Scott Morrison wamehuzunishwa na tukio hilo wakisema ni la kushtua sana.
Wazazi wa Gammy wamenukuliwa katika mjadala na runing moja ya Channel 9 wakisema kuwa wanamtoto mwenye umri wa miezi 6 lakini hawana mtoto mwengine na kukanusha habari kuwa walimtelekeza ndugu ya mtoto wao wa kike.
Wazazi hao wanaoishi mjini Perth, vilevile wameiambia runinga ya taifa kuwa hawajui analosema bi Chanbhua .
Chanbua aliiambia jarida la Fairfax Media kuwa babake Gammy anaumri wa miaka Hamsini hivi na kuwa aliwahi kuja hospitalini na alionekana kumjali sana msichana wake na kumpuuza kabisa Gammy licha ya kuwa alikuwa hapo kitandani.
''Alikataa hata kumtizama usoni mwanaye''
''sasa nitafanya nini ilinipate kumlea ?
Labda itanibidi niwashtaki mahakamani ilinipate hela za kuwatunzia mtoto wao ''.
Waziri wa uhamiaji hata hivyo amesema kuwa serikali ya Australia ikishirikiana na ile ya Thailand zinashirikiana kutafuta suluhu ya mkasa huo .
Bwana Morris alisema kuwa mtoto Gammy ni raiya wa Australia na kuwa anastahili kupata msaada wa kimatibabu kutoka kwa serikali ya Australia.
Ni haramu kumlipa mtu iliakubebee mimba nchini Australia kwa hivyo wazazi ambao hawana uwezo wa kupata mtoto hukimbilia mataifa ya nje na kufanikisha azimio la kuwa wazazi.
Tayari wasamaria wema wamechangisha dola laki mbili kumsaidia mama huyo kumlea mtoto Gammy.

Source:BBC