Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Friday, 5 September 2014

ICC yaahirisha kesi ya kenyatta kwa muda usiojulikana.........

Kiongozi wa mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC, Fatou Bensouda, ameiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa muda usiojulikana.
Hii ni baada ya malalamiko kutoka kwake kuwa Kenya imekataa kushirikiana na mahakama hiyo katika kuikabidhi ushahidi unahitajika kuendesha kesi kwa hiyo ina maana kuwa hana ushahidi wa kutosha dhidi ya Kenyatta.
Katika uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo Fatou Bensouda amesema kuwa hana ushahidi wa kutosha kumfungulia mashitaka Rais Kenyatta ambaye anadaiwa kuhusuika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2007.
Zaidi ya watu 1,000 walifariki katika ghasia hizo. Bensouda amenukuliwa akisema kuwa halitakuwa jambo la busara kufutulia mbali kesi hiyo hasa ikizingatiwa kuwa Kenya haitaki kutoa ushahidi unaohitajika na mahakama hiyo.
Badala yake aliomba mahakama kuiahirisha kesi hiyo hadi pale Kenya itakapokubali kutoa ushahidi unaohitajika.

Source BBC