WAHAMIAJI 26 kutoka nchi jirani za Burundi na Rwanda wamekamatwa juzi katika
Kijiji cha Mlogolo, kilichopo Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ambao kati
yao, 22 ni watoto wenye umri chini miaka 15.
Akizungumzia
tukio hilo,Ofisa Uhamiaji mkoani humo,Andrew Kalengo, alisema wahamiaji
hao walikuwa wakisafirishwa kwenda katika Wilaya ya Chunya,mkoani Mbeya
ili kutumikishwa katika mashamba ya tumbaku.Mkoa wa Kigoma uliopokatika mpaka wa Tanzania na Burundi, hivi karibuni vitendo vya kusafirisha wahamiaji vinaongezeka kwa kasi katika mikoa mingi ukiwemo Tabora jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi," alisema.
Alisema idara yake imejipanga kupambana navitendo hivyo kwa kuongeza doria ili kuwabaini wahamiaji haramu ambao wanatumikishwa na wanaoishi nchini kinyume cha sheria kutoka nchi jirani za Burundi na Rwanda.
"Kuna kikundi chawatu wachache kinachofanya biashara yakuwasafir isha maeneo mbalimbali nchini ilikuwauza kwa watu wanaohitaji vibaruawa kutumikisha katika shughuli zao hususan kilimo cha tumbaku,"aliongeza.
Watoto waliokamatwa Prosper John na Sifa Gwagaza ambao ni raia wa Burundi na Buyoya Lezeri, raia wa Rwanda,walisema hawakujua wanapelekwa wapi na kufanya nini.
"Tulishawishiwa kujaTanzania na kuambiwa kuna kazi nzuri za kufanya...tunaomba kurejeshwa nyumbani,"walisema .
Baadhi yawakazi wa Mkoa huo,wameishauri idara hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,kuwasaka na kuwakamata watu wanaojihusisha na biashara hiyo.
Mtuhumiwa
anayedaiwa kufanya biashara ya kuuza watoto,Bw. Robson Mwendo,alidai
hafanyi biashara ya binadamu bali aliwachukua ili kwenda kuwaajiri
katika mashamba yake .
Dereva wa lori lililobeba wahamiaji hao,Seleman Kagambo, alisema aliwabeba kama abiria hakujua kama ni wahamiaji.