Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Tuesday, 3 March 2015

Pohamba:ndiye mshindi wa tuzo ya Mo Ibrahim kwa mwaka 2014

Rais anayeondoka madarakani nchini Namibia Hifikepunye Pohamba, 79,ameshinda tuzo ya dola milioni tano ya Mo Ibrahimu ya uongozi wa Afrika.
Tuzo hiyo ya dola milioni 5 hutuzwa kiongozi wa Kiafrika aliyechaguliwa na anayeongoza kwa njia bora na kuinua maisha ya watu na kuondoka ofisini

Bwana Pohamba ambaye anaondoka madarakani baadaye mwezi huu ndiye mwanzilishi wa kundi la SWAPO lililopigania uhuru wa Namibia. Rais huyo anatarajiwa kumkabidhi madaraka rais mteule Hage Geingob. Pohamba amehudumu vipindi wili kama rais wa Namibia alipo chaguliwa kwanza mwaka wa 2004 na tena mwaka wa 2009.
Mwanabiashara raia wa Sudan Mo Ibrahim ndiye alizindua tuzo hilo kuwapa motisha viongozi wa Afrika kuondoka madarakani kwa njia ya amani.
Mmoja wa wanajopo wanaoteua marais wanaopewa tuzo hilo Salim Ahmed Salim amemtaja Pohamba kama mtu aliyeiunua maisha ya watu wake
Mshindi anapokea dola milioni 5 ambayo huwa inagawanywa ilikutolewa katika kipindi cha muongo mmoja kisha washindi wanatuzwa dola laki mbili kila mwaka hadi siku ya kufa.