Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Wednesday, 16 July 2014

Habari njema juu ya uwezekano wa kuthibitiwa kwa HIV ifikapo 2030.

Kuna uwezekano kuwa janga la ukimwi huenda likadhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi.
Ripoti hiyo imesema kuwa idadi ya visa vya maambukizi mapya na vifo kutokana na HIV, vimeendelea kushuka.
Na shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.Hata hivyo, shirika hilo linataka juhudi zaidi za kimataifa kufanywa kwani za sasa hazitoshi
Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 35 wanaishi na virusi vya HIV.
Ripoti hiyo ilionyesha visa vipya vya maambukizi milioni 2.1 vilitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2001.
Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.
Afrika Kusini na Ethiopia zimepiga hatua katika kupunguza vifo vya wagonjwa wa HIV.

Source: BBC