Tarehe
10/7/2014 ni siku ambayo Star wa muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania
Diamond Platnumz, ambaye anachafua anga la muziki kwa sasa kwa utunzi na
uimbaji wake alitua katika Uwanja wa Ndege Mwal. Jurius Nyerere, mnamo
mishare ya saa nne na nusu za usiku akitokea nchini Marekani ambapo
alikua huko kushiriki katika Tuzo kubwa Dunia BET awards, ambazo
hufanyika kila mwaka, Diamond alikua katika kategori ya Best African Act
ambayo ilichukuliwa na Davido kutoka Nigeria.
Watanzania
wenye moyo wa Upendo na Kizalendo walijitokeza katika viwanja vya ndege
kumpokea Msanii huyo, wakiwa na mabango makubwa kabisa yenye maneno ya
kuashiria ushujaa aliouonyesha Diamond katika muziki na kuipeperusha
vyema Bendera ya Tanzania katika muziki, Uwanja wa ndege wa Mwl. Julius
Nyerere, uligubikwa na Kelele za Furaha na Sauti zilisikika zikiimba
wimbo wa Mdogomdogo ikiwa ni mapenzi ya dhati kabisa kwa Diamond kwa
kutuwakilisha vema na kurejea salama, hakika kazi ya muziki wetu kwa
sasa inaonekana.
Diamond
baada ya kufika aliwashukuru wote waliofika kumpokea na kusema kuwa
safari yake ilikua nzuri na amejifunza vitu vingi sana pia amekutana na
watu wengi na tutaraji mengine mengi na mazuri katika muziki wetu, na
kwa upande mwingine alitoa shukran za dhati kabisa kwa watanzania
kuipokea vema video yake mpya ya mdogomdogo, imekua ikifanya vizuri sana
na hata youtube imekuwa na views wengi kwa muda mchache
mlinzi wa dimond akisukuma mizigo kwa pembeni DJ Rommy