Jaja akiwa na baadhi ya viongozi wa yanga na baadhi ya mashabiki airport leo
Jaja ambaye alikua akichezea timu ya Itabaina FC nchini Brazil, anakuwa ni mchezaji wa pili kuungana na kikosi cha Young Africans baada ya Andrey Coutinho kuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na kikosi cha kocha Marcio Maximo.
Msemaji wa klabu ya yanga kushoto, Jaja wa katikati na Sefu Magari
Usajili wa wachezaji hawa ni muendelezo wa uongozi wa Young Africans kuhakikisha msimu ujao unakua na kikosi bora ambacho kitaweza kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Kombe la Shrikisho Barani Afrika.
Jaja anaungana na makocha wabrazil Marcio Maximo na Leonardo Neiva na kiungo Andrey Coutinho katikaa msimu huu ambapo kwa pamoja ushirikiano wao na wachezaji wengine wazawa wataisaidia Young Africans kufanya vizuri.
Kesho asubuhi Jaja anatarajiwa kuanza mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ikiwa ni sehemu ya maandaliz ya michuano mbalimbali itayowakabili.