Welcome to my blog!

Meet the Author

Ut eleifend tortor aliquet, fringilla nunc non, consectetur magna. Suspendisse potenti.

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Tuesday, 15 July 2014

Kanisa la Anglikana Uingereza laridhia wanawake maaskofu

Baraza kuu la kanisa la Kianglikana Uingereza, The General Synod, limeidhinisha wanawake kuwa maaskofu. Maafisa katika kanisa hilo wanaamini wana ufuasi mkubwa unaounga mkono hoja hiyo. Makasisi wanawake walio thuluthi moja ya viongozi wa kidini wa kanisa la kianglikana, wanasema haki sawa itawapandisha hadhi katika makanisa.Sasa baada ya kupitishwa kwa kura hiyo, huenda askofu wa kwanza mwanamke akachaguliwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
 Hatua hiyo inemaliza mvutano wa miaka mingi na kuvunja utamaduni wa makarne katika kanisa hilo. Tofauti nyingi zimeibuka kuhusu suala hilo na hata kusababisha migawanyiko katika kanisa hilo ambapo baadhi ya ma dayosisi yameshawatawaza maaskofu wanawake, na kukaidi amri la hapo awali la kanisa kuu. 
Nchi zilizo na maaskofu wanawake:New Zealand,Australia,Marekani,Canada na Afrika Kusini 'Msimamo wa viongozi wa kanisa hilo Afrika'
Kasisi Moses Bushendich kutoka kanisa la Kianglikana Uganda ameambia BBC kuwa misimamo imegawanyika juu ya maaskofu wanawake kutokana na mafundisho ya Bibilia.  ''Kanisa la Afrika halina uamuzi wa pamoja juu ya suala hili. Kila tawi limechukua msimamo wake baadhi wanapinga na wengine wanaunga mkono'' amesema kasisi Bushendich.
Baadhi ya itikadi ambazo zimekuwepo kwa miaka mingi katika makanisa makuu kama vile Katoliki na Anglikana ni wanawake kuwa maaskofu wanawake, na kuruhusu ndoa ya wapenzi wa Jinsia moja ambayo tayari baadhi ya maumini na maaskofu wa kanisa hilo wamepigia debe kuidhinishwa.

SOURCE: BBC