Idara ya Uhamiaji Nchini, imewakamata Raia wa nane (8) wa kigeni wakati
wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere,
wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya.
Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014
majira ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la Ndege la
Uturuki yenye Namba TK 603, wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa
Raia wa Sweden na Belgium.
Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia
ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu
kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.
kukamatwa kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji
haramu nchini ambapo suala la Udhibiti wa Mipaka linapewa kipaumbele.
akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu
Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji
wanaendelea kufanyakazi usiku na mchana kuhakikisha Sheria
na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa. "Idara ya Uhamiaji, iko macho
hatulali kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa nchi ikiwa ndio jukumu letu
namba moja unaimarika. kwahivyo, kila mtu awe Raia wa kigeni na
Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na Taratibu zilizopo za kuingia na
kutoka nchini"
Hadi sasa, Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea kushikiliwa
na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri kurudishwa
walikotoka. Hili ni wimbi lililoibuka hivi karibuni kwa baadhi ya Raia
wa nchi za Iraq, Iran, Syria kujaribu kuingia nchini isivyo halali huku
ikisemekana lengo lao kubwa ni kuingia Tanzania na baadae kutoka
kuelekea Mataifa ya Ulaya.
Majina ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina
halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye
mabano ni kama ifuatavyo;
1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)
2. SAMER HELMI KAMIT - SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
4. DAVID GABRIEL POBLETE - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
5. SADDAM ALKHAMERI AREF - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
8. ALI HUSSEIN OLEIWI - IRAQ, PPT. NO. G 1111623