Jaycee Chan, 31, ambaye mwenyewe ni msanii pamoja na muigizaji kutoka Taiwanese Kai Ko, 23, walikamatwa alhamisi iliyopita kwa mujibu wa taarifa ya polisi mjini Beijing .
Polisi wanasema kuwa wawili hao walipatikana wamevuta bhangi huku mwanawe Chan akikabiliwa na kosa zaidi la kupatikana na dawa hiyo haramu.
Kukamatwa kwa wawili hao kunawadia wakati polisi wamekuwa wakifanya misako ya dharura na kuwakamata wasanii nyota kadhaa.
Gao Hu, 40, aliyeigiza katika filamu ya mwaka wa 2011 Zhang Yimou "The Flowers of War", alikuwa miongoni mwa wasanii wengine wakutajika waliokamatwa mapema mwezi huu.
HU alipatikana ametumia Bhangi pamoja na madawa aina ya methamphetamines.
Operesheni hizi zinafuatia agizo la rais wa China Xi Jinping mwezi juni kwa polisi la kuwataka kuimarisha juhudi za kukabiliana na matumizi ya mihadarati nchini humo.
Duru zinaarifu kuwa Kukamatwa kwa mwanawe msanii maarufu zaidi nchini humo maafisa wa polisi wanajaribu kuwadhibitishia umma kuwa hakuna atakayeepuka mtego wao .
"ikiwa tutaendelea na kampeini hii dhidi ya matumizi ya mihadarati ninahakika waigizaji wengi nyota watakamatwa ''
Juma lililopita miungano 42 inayowakilisha wasanii walitia sahihi maagano ya kukataa kuwasajili wasanii waotumia mihadarati katika maonesho yao.
Kampuni inayomwakilisha bwana Chan iliomba msamaha kwa uma kwa niaba yake.
Kampuni hiyo ya M'Stones International iliahidi kumpeleka hospitalini ilikukomesha matumizi ya dawa hizo.
Babake Jackie Chan hajasema lolote kufikia sasa.