Wanajeshi 480 wa Nigeria
wametorokea maisha yao nchi jirani ya Cameroon kufuatia makabiliano
makali dhidi ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram.
Msemaji wa jeshi la Cameroon Luteini Kanali
Didier Badjek amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa wamepokonywa
silaha na sasa wamewekwa katika shule .
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau
alizungumza kwenye kanda ya video iliyotolewa ili kupongeza wapiganaji
wake kwa kuchukua udhibiti wa mji wa Gwoza mapema mwezi huu.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria Chris Olukolade alipinga tangazo hilo akisema kuwa ''hakuna hata nchi moja ya taifa hilo iliyotwaliwa na kuwa Nigeria ni moja. ''
Imepeperusha bendera zake juu ya Kasri ya Emir wa Gwoza, kiongozi wa kiasili wa mji huo, wakazi wanasema.